Rais Dkt. Samia ashiriki mkutano kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi jijini Addis Ababa nchini Ethiopia
JamhuriComments Off on Rais Dkt. Samia ashiriki mkutano kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi jijini Addis Ababa nchini Ethiopia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki mkutano wa Kamati ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (CAHOSCC) kando ya Mkutano wa Kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU), Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 16 Februari, 2025.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mwenyekiti wa Kamati ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (CAHOSCC), Rais wa Kenya Mhe. William Ruto kando ya Mkutano wa Kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU), Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 16 Februari, 2025.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Mkutano wa Kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) kwa niaba ya Mwenyekiti wa AU, Rais wa Angola Mhe. João Lourenço katika ukumbi wa Nelson Mandela uliopo Makao Makuu ya Umoja huo, Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 16 Februari, 2025. Aidha, Tanzania imechaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Uongozi wa Umoja wa Afrika (Bureau of the African Union Assembly) kwa mwaka 2025.