Rais Dkt. Samia aendelea na Ziara yake ya Kikazi wilayani Pangani Mkoani Tanga
JamhuriComments Off on Rais Dkt. Samia aendelea na Ziara yake ya Kikazi wilayani Pangani Mkoani Tanga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi na ugawaji wa Boti kubwa za kisasa 120 pamoja na boti saidizi 118 kwa nchi nzima. Kwa upande wa Mkoa wa Tanga, Rais Mhe. Dkt. Samia amekabidhi boti kubwa 30 kati ya 35 pamoja na boti saidizi 60 kwenye hafla iliyofanyika Pangani mkoani humo tarehe 26 Februari, 2025.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia wananchi wa Wilaya ya Pangani kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa kumba ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi mkoani Tanga tarehe 26 Februari, 2025.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Bagamoyo (Makurunge)-Pangani -Tanga (km 256) sehemu ya Mkange-Pangani-Tanga (170.8) pamoja na Daraja la mto Pangani (M525) kwenye hafla iliyofanyika Pangani mkoani Tanga tarehe 26 Februari, 2025. Muonekano wa Daraja la muda linalotumika kupitisha vifaa kwa ajili ya ujenzi sambamba na ujenzi wa nguzo za Daraja la mto Pangani ukiendelea Wilayani mkoani Tanga, tarehe 26 Februari, 2025. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akionesha sehemu linapojengwa Daraja la mto Pangani (M525) mara baada ya kuzindua Boti kubwa za kisasa 120 pamoja na boti saidizi 118 kwa nchi nzima katika eneo la Bandari ya Pangani mkoani Tanga tarehe 26 Februari, 2025.Muonekano wa boti za Uvuvi pamoja na za boti za kilimo cha Mwani kabla ya kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Pangani mkoani Tanga tarehe 26 Februari, 2025.