Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitoa Tuzo ya Mkapa kuhusu Uongozi thabiti kwa Washindi mbalimbali kutoka Sekta ya Afya Nchini. Mhe. Rais Samia alitoa Tuzo hizo wakati wa kilele cha Kumbukizi ya 3 ya Urithi wa Mkapa katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Julai, 2024.