Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani ameweza kutekekeza miradi yote ya kimkakati iliyoasisiwa na watangulizi wake  ikiwemo  ya Rais wa Awamu ya Tano, Dkt. John Pombe Magufuli.

Amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia  ametimiza ahadi aliyoitoa kwa Watanzania mara alipoingia madarakani ya kuwa hakuna mradi utakaosimama chini ya uongozi wake na kwamba ataendeleza kila kilichoanzishwa na watangulizi wake.

Amesema hayo leo Jumanne (Machi 18, 2025) alipozungumza katika Kongamano la kumpongeza Mheshimiwa Rais DKt. Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio ya miaka minne ya uongozi wake  lililoandaliwa na Waandishi wa Habari Mahiri wa Mkoa wa Mwanza kwenye ukumbi wa Tunza jijini Mwanza.

Mheshimiwa Majaliwa amesema Rais  Dkt. Samia alipotoa hotuba yake ya kwanza bungeni  aliahidi kuwa miradi yote itaendelezwa na mingine mipya  itaanzishwa.

Mheshimiwa Majaliwa amesema Rais Dkt. Samia amefanikiwa kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo pamoja na ya huduma za jamii inayowagusa wananchi wote hadi vijijini kwenye sekta za afya, elimu na maji “wote ni mashahidi wa mafanikio makubwa ambayo yamefikiwa na Serikali katika utekelezaji wa miradi hiyo”

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  katika Kongamano la Kumpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio ya miaka minne ya uongozi wake lililoandaliwa na Waandishi wa Habari Mahiri  wa Mkoa wa Mwanza katika  ukumbi wa Tunza jijini Mwanza, Machi 18, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Kuhusu sekta ya  maji Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa hivi sasa Serikali inatekeleza miradi kwenye maziwa, mito na Mabwawa kwa ajili ya kuwapelekea wananchi wenye uhitaji wa maji safi na salama katika maeneo mbalimbali nchini.

Aliitaja mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Tabora, Singida, Dodoma na Mara  kuwa  itakayonufaika na miradi wa maji ya Ziwa Victoria  Alisema miradi kama hiyo iko pia katika mikoa ya Geita na  Kagera.

Kuhusu afya Mheshimiwa Majaliwa amesema  Serikali imewekeza katika miundombinu ya kutolea huduma za afya, dawa na vifaa tiba kuanzia ngazi  ya kata hadi Taifa, lengo likiwa ni kusaidia kupunguza adha kwa wananchi kutembea umbali mrefu kupata huduma za afya ikiwemo za kibingwa.

Kuhusu nishati ya umeme amesema wilaya na vijiji vyote vimepatiwa umeme na hivi sasa Serikali inasambaza umeme kwenye vitongoji na visiwa ili  kuhakikisha kwamba kila nyumba anamoishi Mtanzania  inafikiwa na huduma ya umeme.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na vingozi  alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mwanza ambako alikuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Kumpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio ya miaka minne ya uongozi wake lioandaliwa na Waandishi wa Habari Mahiri wa Mkoa wa Mwanza  katika  ukumbi wa Tunza jijini Mwanza, Machi 18, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Akizungumzia kilimo Mheshimiwa Majaliwa amesema zao la pamba ambalo awali uzalishaji wake ulikuwa umezorota Serikali  imeimarisha mifumo ya masoko ya zao hilo kwa kuanzisha mfumo wa stakabadhi ghalani ambao umepandisha bei ya zao kilo.

Amesema hivi sasa zao la hilo limerudi kwenye nafasi yake  ya kuwa moja kati ya mazao makuu  ya biashara nchini na viwanda vingi vya kuchambua pamba vimejengwa  hasa mkoani Simiyu. 

Kuhusu  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuteuliwa kuwa mgombe wa Urais wa CCM Katie uchaguzi mkuu ujao, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa amefurahishwa na kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza  Michael Lushinge kuwa mkoa huo utaongoza tena kwa kumpiga kura nyingi za ndiyo mgombea Urais  wa CCM. 

Akitoa mada katika kongamano hilo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania,  Masanja Kagosa amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alianzia Kanda ya Ziwa kwa kuweka jiwe la msingi  la ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR ya kutoka Mwanza kwenda Isaka lengo likiwa ni kuifanya Mwanza kuwa kitovu cha biashara kwa Ukanda wa Maziwa Makuu.

Naye Mratibu wa kongamano hilo, Aloyce Nyanda amesema kuwa  kwa namna yoyote kazi zinazofanywa na Serikali zina manufaa makubwa kwa wananchi ndiyo maana yeye na waandishi wenzake wa habari wameamu kujadili mafanikio ya miaka minne ya uongozi wa  Rais Dkt. Samia  kama kiongozi wa mkuu wa nchi na mtumishi wa watu.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mwanza ambako alikuwa mgeni rasmi katika  Kongamano la Kumpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio ya miaka minne ya uongozi wake ililoandaliwa na Waandishi wa Habari Mahiri wa Mkoa wa Mwanza  katika  ukumbi wa Tunza jijini Mwanza, Machi 18, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Kumpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio ya miaka minne ya uongozi wake lililoandaliwa na Wandishi wa Habari Mahiri wa Mkoa wa Mwanza  kwenye ukumbi wa Tunza jijini Mwanza, Machi 18, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)