Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani ulioongozwa na Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Aprili,2025.

Rais Dkt. Samia pamoja na viongozi hao wamejadili kuhusu utoaji wa huduma kwa watoto wenye mahitaji maalum hususan wenye changamoto ya afya ya akili. Viongozi hao wa Kanisa wameipongeza na kuishukuru Serikali kwa ushirikiano inaotoa kwa Kanisa hilo.

Aidha, kuhusu utoaji wa huduma kwa watoto wenye mahitaji maalum hususan wenye changamoto ya akili, Serikali imeahidi kushirikiana na Kanisa ili kujenga Kituo kikubwa zaidi ili watoto wengi waweze kupata huduma hiyo.