Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi atashiriki Uzinduzi  wa Usafiri wa Treni ya Umeme kwa kutumia Reli ya Kisasa (SGR).

Uzinduzi wa mradi wa SGR utafanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusafiri na treni hiyo safari yenye umbali wa kilomita zaidi ya 400 ambayo inatarajiwa kuanza jijini Dar es Salaam  mosi Agosti.