Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa pamoja na viongozi wengine wakati akivuta kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi mradi wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Bandari za Ziwa Tanganyika (Kibirizi na Ujiji) katika Sherehe zilizofanyika Kibirizi Mkoani Kigoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa pamoja na viongozi wengine wakati walipotembelea eneo la Bandari ya Kibirizi katika Ziwa Tanganyika mara baada ya kuweka jiwe la Msingi mradi wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Bandari za Ziwa Tanganyika katika Sherehe zilizofanyika Kigoma mjini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Kibirizi mara baada ya kuweka jiwe la Msingi mradi wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Bandari za Ziwa Tanganyika katika Sherehe zilizofanyika Kibirizi Mkoani Kigoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel akiangalia mashine ya (MRI) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni Kigoma mara baada ya kuweka  jiwe la Msingi Jengo la kutolea Huduma za Wagonjwa wa Dharura (EMD) na Wagonjwa Mahututi (ICU) Katika Hospitali hiyo