Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambae pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ akishiriki Mkutano wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya hiyi (SADC Organ) kwa njia ya mtandao, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 06 Machi, 2025. Mkutano huo umejadili masuala ya hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.