Rais ashiriki mkutano wa dharura wa SADC kwa mtandao
JamhuriComments Off on Rais ashiriki mkutano wa dharura wa SADC kwa mtandao
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ) Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC kwa njia ya Mtandao pamoja na viongozi mbalimbali, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 13 Machi, 2025. Mkutano huo pamoja na mambo mengine unajadili hali ya ulinzi na usalama Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).