Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akielekea katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja, kuhudhuria Kongamano la Kiimani Kwa Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, lililofanyika katika Ukumbi huo leo.23-3-2025, (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Dkt. Haroun Ali Suleiman na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa.(Picha na Ikulu)

BAADHI ya Viongozi wa Serikali na Taasisi za Serikali wakifuatila Mada zikiwasilishwa katika Kongamano la Kiimani kwa Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja leo 23-3-2025.(Picha na Ikulu)

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akifuatilia Mada zikiwasilishwa katika Kongamano la Kiimani kwa Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja lililofanyika leo 23-3-2025 na (kulia ) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Kiongozi.(Picha na Ikulu)

SHEIKH. Nurdin Kishki kutoka Jijini Dar es Salaam akiwasilisha mada ya Kuwatii na Kuwathamini Viongozi ni Msingi wa Kuwepo kwa Amani Nchini, wakati wa Kongamano la Kiimani kwa Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja leo 23-3-2025.(Picha na Ikulu)

Sheikh Farid Hadi kutoka Zanzibar akiwasilisha mada  ya Uvunjifu wa Amani ni Sababu ya Kuporomoka kwa Uchumi, wakati wa Kongamano la Kiimani kwa Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja leo 23-3-2025.(Picha na Ikulu)

Sheikh Dr. Mbaraka Awesu kutoka Kenya akiwasilisha mada ya Zaka ni Suluhisho la Umasikini Ikitolewa Ipasavyo, wakati wa Kongamano la Kiimani kwa Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja leo 23-3-2025.(Picha na Ikulu)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza  katika Kongamano la Kiimani kwa Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, lililofanyika leo 23-3-2025  katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakili Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi mbalimbali katika kuitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaab (kushoto kwa Rais) baada ya kumalizika kwa Kongamano la Pili la Kiimani kwa Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, lililofanyika leo 23-3-2025 katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)