Muungano mkuu wa upinzani nchini Kenya umetangaza mipango ya kufanya”mazungumzo ya moja kwa moja” na umma wakati ukijiandaa kwa mazungumzo na serikali kuhusu mageuzi kuhusu uchaguzi.
Muungano huo wa Azimio la Umoja, unaoongozwa na mwanasiasa mkongwe wa upinzani Raila Odinga, ulisema kuwa bado unajitolea kuepusha wasi wasi wa kisiasa kwa njia ya mazungumzo baada ya maandamano ya kuipinga serikali yaliyogeuka kuwa ghasia mwezi uliopita.
Muungano huo umesema kuwa utafanya mkutano wake wa kwanza wa kusikiliza maoni ya umma siku ya Alhamisi ambao utafuatiwa na mkutano wa hadhara Jumapili katika mji mkuu Nairobi na hatua zitakazochukuliwa”.
“Azimio bado imejitolea katika moyo wa mkataba wa Pasaka ambapo pande mbili ziliafiki kufanya mazungumzo ,” ilisema taarifa ya Azimio la Umoja.
Muungano tawala na Azimio tayari zimekwishataja majina ya wawakili wao katika mazungumzo, ambayo Bw Odinga anasema ni lazima yaendelezwe zaidi ya bunge.
Upinzani unaitaka serikali “kuja kwenye meza ya mazungumzo na mikono safitsafi, bila hasira na kuwa tayari kwa mchakato wa kweli n awa uwazi wa kuzungumzia matatizo yanayoikumba nchi”.
Mwezi uliopita , watu watatu , akiwemo ofisa wa Polisi, walifariki na mali kuharibiwa katika maandamano ya kupinga serikali ambayo pia yaliajeruhi mamia ya watu wengine.
Bw Odinga, ambaye anadai kwamba aliibiwa kura za urais katika uchaguzi wa mwaka jana , alisitisha maandamano baada yar ais William Ruto kukubali kufanya mazungumzo na upinzani.
Ametishia kurudi mtaani iwapo Azimio haitaridhishwa na mchakato