Na Jumanne Magazi, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Rais Dk.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara nchini Uturuki kwa lengo la kukuza uhusiano wa kidiplomasia ya siasa, uchumi, na biashara kati ya nchi hizo.
Akizungumza leo Aprili, 15 jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amesema Rais Dk,Samia anafanya ziara hiyo baada ya Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan kumpa mwaliko wa kutembelea nchini humo.
Amesema ziara hiyo ni kubwa na ya kihistoria nchini kwetu ambayo itaanza April 17 hadi Aprili 21 mwaka huu.
“Nchi ya Uturuki ni moja nchi ipo kwenye kundi la nchi 20 wanaofanya vizuri hivyo tunajua ziara hiyo itakuwa ya kimkakakti nchini kwetu,”amesema Makamba.
Ameeleza kuwa lengo lingine la kufanya ziara hiyo ni kupata mtaji na teknolojia ambao nchi ya Uturuki wanayo , kupata masoko ya bidhaa ambayo yapo nchini humo na kupata wawekezaji kwa lengo la kuwekeza nchini.
Amesema tayari wameshaona makampuni makubwa kutoka Uturuki wakifanya shughuli.