Na Fredy Mgunda, JamhuriMedia, Nachingwea

Mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Kipaumbele , Alex Justine (18), wilayani Nachingwea amefariki baada ya kupigwa na radi akiwa darasani akifanya mtihani wa kujipima kwa ngazi ya wilaya.

Akidhibisha kutokea kwa kifo hicho Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mohamed Hassan Moyo, amesema kuwa ni kweli radi imesababisha kifo cha mwanafunzi mmoja na wengine 44 kujeruhiwa.

Moyo amesema kuwa majeruhi hao walikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Nachingwea na kupatiwa huduma ya kwanza.

Kaimu Mganga mkuu Dkt.Ramadhan Maige amesema kuwa majira ya saa 9.30 alipokea simu kutoka kwa Afisa Elimu Sekondari juu ya kutokea kwa ajali hiyo iliyotokana na radi.

Dkt.Maige amesema kuwa walipokea majeruhi 45 kutoka katika shule ya Sekondari Kipaumbele huku mwanafunzi mmoja akiwa tayari ameshafariki.

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alipotembelea wanafunzi wa shule ya sekondari Kipaumbele waliojeruhiwa na radi
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiwafariji wazazi wa marehemu Alex Justine baada ya kuelezwa kuwa mtoto wao amefariki kutokana na ajali ya radi.
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alipotembelea wanafunzi wa shule ya sekondari Kipaumbele waliojeruhiwa na radi.
Please follow and like us:
Pin Share