Washington: Utumwa unanikera
“Ninaloweza kusema ni kwamba hakuna mtu aliye hai mwenye kutamani kwa dhati kuona utumwa unakomeshwa zaidi yangu.”
Haya ni maneno aliyoyasema Rais wa Kwanza wa Marekani, George Washington, wakati wa harakati wa kulipatia taifa hilo uhuru kutoka kwa Waingereza. Marekani ilipata uhuru wake mwaka 1776.
****
Kaiser: Hakuna bahari bila Ujerumani
“Ukubwa wa Ujerumani unaifanya isiweze kuwapo bila kuwa na bahari, lakini pia bahari yenyewe inathibitisha kuwa hata kwa umbali gani, na kwa upande mwingine bila Ujerumani na Mfalme wa Ujerumani, hakuna uamuzi wa maana unaoweza kufanyika.”
Haya ni maneno ya aliyekuwa Mfalme wa Ujerumani, Kaiser Wilhelm II (William II) wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Hapa alikuwa akieleza ukuu wa Ujerumani katika dunia ya wakati huo.
*****
Mackenzie King: Tumefanya makubwa
“Tumekamilisha mengi kwa jamii na maendeleo ya binadamu kwa kuzuia mabaya mengi kwa njia ya kutenda mema.”
Haya ni maneno ya Waziri Mkuu wa Kwanza wa Canada, William Lyon Mackenzie King, aliyetawala kati ya Desemba 1921 na 1948.
*****
Nassar: Lazima ujiweze kwanza
“Mtu asiyejiweza yeye binafsi, hawezi hata kufanya uamuzi.”
Haya ni maneno ya aliyekuwa Rais wa Misri, Gamal Abdel Nasser, alipokuwa akichagiza Wamisri kujenga utamaduni wa kujitegemea.