Putin amewataka wajitolea wote “wanaofanya kazi za kijeshi” kula kiapo mbele ya bendera ya Serikali ya Urusi.
Alitoa amri ya kuomba kiapo hicho, ambacho kinawafaa wale wanaoshiriki katika shughuli za kijeshi nchini Ukraine, kusaidia jeshi, pamoja na raia wanaohudumu katika vitengo vya ulinzi wa eneo, shirika la habari la serikali la Urusi TASS liliripoti.
Haijabainika wazi kabisa maana ya kiapo hicho, lakini ilifika wakati wapiganaji mamluki wa Wagner wakikosa kiongozi dhahiri.
Wiki chache kabla ya ghasia za Prigozhin kushindwa mwezi Juni, Wizara ya Ulinzi ya Urusi iliyapa makundi ya mamluki muda hadi tarehe 1 Julai kusaini mikataba.
Prigozhin alikataa kutia saini, kwa sababu hakutaka Kundi lake la Wagner lifanye kazi chini ya wizara.
Putin aliunga mkono mpango wa kandarasi wa wizara hiyo wakati huo, ambalo lilikuwa pigo la kwanza la umma dhidi ya mshirika wake wa muda mrefu Prigozhin.