Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda leo Septemba 2, jijini Dar es Salaam amekutana na kufanya mazungumzo na balozi wa Singapore nchini Bw.Douglas Foo.

Katika mazungumzo hayo Tanzania na Singapore zimekubaliana kuboresha ushirikiano zaidi katika sekta ya elimu ikiwemo kubadilishana uzoefu kwa walimu na wakufunzi kutoka taasisi za elimu za nchi hizo.

Akizungumza katika kikao hicho Prof.Mkenda amesema mfumo wa elimu nchini Singapore umewezesha kupambana na tatizo la ajira katika nchini humo, hivyo Tanzania itapata uzoefu huo kupitia timu zinazohusika na uboreshaji Sera na mabadiliko ya mitaala.