Na Andrew Chale, JamhuriMedia, Zanzibar.
MWANAMAJINUNI wa Afrika, Profesa Patric Loch Otieno Lumumba ambaye pia akifahamika kama Prof. PLO Lumumba ametoa rai kwa sanii Vijana wa Afrika hususani Afrika Mashariki kutumia jukwaa la tamasha la Nchi za Jahazi (ZIFF) katika kuandaa filamu za ubunifu na zenye tija.
Prof. PLO Lumumba ameyasema hayo katika ujumbe wake aliowasilisha kwa njia ya video wakati akiwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu ni la 26, tokea kuanzishwa kwake huku filamu zaidi ya 90 zikionyeshwa katika maeneo tofauti ya Visiwa vya Pemba na Unguja, Zanzibar.
Ambapo amewataka Vijana hao kuwa mbele katika kuipa harakati sekta ya ubunifu wa kutengeneza filamu.
“Muacha Mira ni mtumwa, sisi Waafrika tunatambuliwa na kuchukuliwa kama wasanii wazuri, Wabunifu wazuri,
Lakini kwa muda wa miaka mingi tu hatujatumia fursa hiyo kuhakikisha kwamba tumejiendeleza inavyostahili.
Tamasha kama hili la ZIFF inatupa fursa ya kutathimini na kujiuliza maswali mengi ya kujielimisha na kujihamasisha” Amesema Prof. PLO Lumumba.
Na kuongeza: “Nachukua fursa hii kuwaelezeni Waafrika kuwa wakati ni huu waafrika kujipiga moyo konde kwa kuchukua hatua za makusudi ili kuhakikisha kwamba, ubunifu umepewa kipaumbele, vijana wa Afria ni wengi tu ambao wana uwezo na sifa na ‘tajiriba’ ya kuhakikisha wanaendeleza ubunifu na sisi ambao tupo hapa na wengine wa nje (Diaspora) na wengineo wanauwezo wa kuwasaidia waafrika katika kuhakikisha wanakuwa wananaharakati wa kusaidia kuwapa ubunifu, mfano Nchi ya Nigeria, wanapata pesa nyingi kupitia soko lao la filamu za Nollywood,
Sasa Kanda hii ya Afrika Mashariki na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnafursa ya kipekee kuhakikisha kwamba vijana wetu hasa wasanii wamehamasishwa, mie nikiwa mdogo nilimsikiliza sana muimbaji mashuhuri Baraka Mwishehe Mwaruka, na Baraka alisifika sana kwa uhodari wake na uimbaji wake,
Ni wakati wa kuhakikisha kwanba tumewapa fursa akina vijana Mwishehe Mwaruka mambo leo ilikuibuka kuhakikisha kwamba wamepewa fursa ya kuwaajiri wengine, ninahakika ya kwamba tamasha hili wale wameudhuria watawapa vijana hawa wosia unaofaa na hata wazee wanaoshiriki katika ubunifu, na Serikali pia inajukumu la kuwafadhiri vijana hawa na taasisi na asasi husika kuhakikisha usanii na ubunifu umepewa kipaumbele na unanoga jinsi unavyostahiri.” Amemalizia Prof. PLO Lumumba.
Katika ufunguzi huo, filamu ya
Married to work iliweza kufungua pazia ya filamu 90 ambazo zitaoneshwa kwa siku 10, Juni 24 hadi Julai 2, mwaka huu.