Na Magrethy Katengu, JamuhuriMedia
Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi Taifa (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema kutoka na hali halisi inayoendelea kila nchi inaonyesha kuwa demokrasia inaendelea kuporomoka duniani.
Prof.Lipumba aliyasema hayo leo Januari 7,2025 jijini Dar es Salaam wakati akifungua Kikao Cha Baraza Kuu la Chama hicho ,ambapo amesisitiza kuwa jukumu la kulinda demokrasia hapa nchini ni kila mtu anahusika na Watanzania wote ni budi kutambua umuhimu wa jambo hilo.
Profesa Lipumba amebainisha kuwa licha ya juhidi ya za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kurudisha hali ya maridhiano ya kisiasa laki bado hali haijawa sawa kwa Tanzania Demokrasia inaendelea kuporomoka hiyo imejidhihirisha katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliyofanyika mwaka 2024 hivyo amemuomba kitimiza jukumu la kuhakikisha dosari zilizojitokeza katika uchaguzi huo wa 2024 na 2020 zisijitokeze tena katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu 2025.
” Hali ya Demokrasia Duniani ilikua ikiporomoka ,wataalamu wa mambo ya Demokrasia wanaonesha katika tafiti tangu mwaka 2006 ,Demokrasia imekua ikiporomoka Duniani hasa ikiangaliwa uchaguzi wa Marekani huko nako hali ni mbaya ” amesema Prof.Lipumba.
Amesesitiza kuwa Marekani ambapo pamoja na mapungufu mengi ndiko utaratibu wa demokrasia ulipoanza kwa kuweza kuchagua viongozi wa kuwawakilisha wananchi nako demokrasia imekua ikiporomoka siku hadi siku.
Profesa Lipumba meongeza kuwa hata uchaguzi uliopita wa Marekani wa kumchagua Rais Donald Trump ambaye Mwaka 2020 aliyakataa matokeo ya uchaguzi inaonesha namna Demokrasia ilivyoporomoka nchini humo.
Aidha Profesa Lipumba amebainisha kuwa kutokakana na kuonekana kuporomoka Demokrasia nchini,amemsihi Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kusimamia falsafa yake ya 4R ili Demokrasia nchini iendelee kuimarika.