Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia,Dodoma

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Prof. Mohamed Janabi amezishauri Klabu za soka nchini kufanya uhakiki wa afya za wachezaji kabla ya kuwasajili kuepuka kupoteza gharama pindi wanapopata madhara kiafya.

Prof. Janabi ameeleza hayo leo Agosti 10,2023 Jijini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa utekelezaji wa majukumu ya hospitali hiyo ya taifa mwaka wa fedha 2023/2024.

Amesema kumekuwa na matukio ya wachezaji kuanguka uwanjani na kupoteza maisha kutokana na matatizo ya maradhi mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa moyo jambo linalopaswa kitizamwa zaidi.

“Vifo vingi vya wachezaji vinavyotokea uwanjani mara nyingi vinatokokana na ugonjwa wa moyo,hii ni kutokana na tabia ya kutofanya uchunguzi wa afya zetu mara Kwa mara,lazima tuwe na utaratibu wa kujua afya zetu,”amesema na kuongeza;

Nashauri Viongozi wa Klabu kuwa na utaratibu wa kuwapima wachezi kabla ya kuingia nao mkataba ,usajili unatumia gharama kubwa ,”amesisitiza

Katika hatua nyingine Prof.Janabi ameeleza kuwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ina mpango wa kuendelea kutoa huduma za Kibingwa na Ubingwa Bobezi ikiwemo Kuanzisha huduma za kupandikiza mimba, figo, uloto na vifaa vya usikivu Kukamilisha upembuzi yakinifu wa kuimarisha huduma za uchunguzi.

Amesema Kwa kipindi cha mwaka wa fedha uliopita wa 2022&2023 imetoa huduma kwa njia ya msamaha zenye thamani ya TZS 18,264,312,466, sawa na wastani wa TZS 1,522,026,038 kwa mwezi.

Misamaha hii inatokana na vipimo maabara (4%), vipimo radiolojia (0.2%), Dawa (82%), kulala (0.2%), huduma za ICU (0.1%) n.k 7.0 Kuimarika Utendaji wa Huduma Hospitali ya MNH MloganzilaTarehe 03 Oktoba 2018, Serikali iliagiza Hospitali hiyo kuwa chini ya usimamizi na uendeshaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) hivyo kwa sasa inaitwa, Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila.

Pamoja na hayo amesema jumla ya Wagonjwa 6,200 wanaonwa kwa siku katika Hospitali zote mbili ambapo kwa upande wa Upanga, wagonjwa 3,800 wanahudumiwa kwa siku ikiwa ni wagonjwa wa nje 2,500 na wagonjwa 1,300 ni wagonjwa waliolazwa wodini wakati wote.

Prof.Janabi amesema ,”Muhimbili ikiwa ni Hospitali ya Rufaa ya Kitaifa na kubwa kuliko zote nchini ina vitanda 2,150 ambapo Upanga kuna vitanda 1,550 na Mloganzila vipo 600 huku Mloganzila ikiwa inahudumia jumla ya wagonjwa 1,400 kwa siku sawa na wagonjwa wa nje 900 na wagonjwa 500 waliolazwa,”amesema.

Kuhusu kupunguza msongamano wa watu Muhimbili, alifafanua kuwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ilifanya tathimini na kubaini kuwa kwa siku moja eneo hilo wanaingia watu 20,000 na magari 3,500 na kwamba hali hiyo imekuwa changamoto kwani ndugu wa wagonjwa na wafanyakazi walikua wakikosa mahali pa kuegesha magari yao.

“Tathimini hiyo ilionesha kuwa kuna baadhi ya watu wanaegesha magari yao ndani kutokana na usalama uliopo, kutokuwepo mfumo wa malipo ya maegesho ambapo wakishaegesha huenda kufanya shughuli zao Kariakoo au mjini,

Hali hii ilitulazimu kuanzisha utaratibu wa kulipia huduma ya maegesho ili isaidie kupunguza msongamano wa magari ndani ya Hospitali,”alisema.

Ameongeza kuwa jitihada za kupunguza msongomano Upanga ziligusa pia kuhamisha huduma tatu kwenda Mloganzila kwa lengo lile lile la kupunguza msongamano mkubwa uliokuwepo MNH Upanga na kupunguza idadi ya ndugu wanaokuja kusalimia wagonjwa waliolazwa kutoka watano kwa wakati mmoja hadi wawili asubuhi, mmoja mchana na wawili jioni.

Amesema,”uratibu huu unalinda watumiaji wa huduma wakiwemo wagonjwa na wageni wote wanaongia wanaoingia na kutoka ndani ya Hospitali,”amesema

Please follow and like us:
Pin Share