Na Mwandishi wetu, JakhuriMedia, Dar es Salaam
Ikiwa imesalia siku kadhaa kuelekea sikukuu ya Pasaka ambayo itaanza maadhimisho yake siku ya Ijumaa Kuu Machi 29, 2024 na baadae kufuatiwa na mkesha sikukuu yenyewe wananchi wameombwa kutoa taarifa za viashiria au dalili za kihalifu ili wahusika washughulikiwe mapema .
Akizungumza leo Machi 28,2024 Kamanda wa Jeshi la Polisi Dar es Salaam Jumanne Muliro ametahadharisha umma kuhusu usalama kuelekea mchezo wa Soka kati ya Simba Vs Al Ahly na Yanga Vs Mamelodi Sundowns.
Sambamba na hayo amebainisha kuwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam litakuwepo kuanzia Ijumaa 29 Machi 2024 na Jumamosi 30 Machi 2024 majira ya saa 3 usiku kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam kutakuwa na michezo ya soka ya ligi ya mabigwa Afrika kati ya timu ya Simna ya Tanzania na AL Ahly ya Misri utakaochezwa kuanzia saa 3:00 usiku.
Pia tarehe 30 Machi 2024 mchezo kati ya timu ya Yanga ya Tanzania na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Hata hivyo kuuelekea michezo hiyo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limechukua tahadhari zote za kiusalama kabla, wakati na baada ya mchezo.
Usalama siku ya mchezo utakuwa wa kiwango cha juu, maeneo yanayozunguka uwanja ndani, nje na barabara za kuingia na kutoka uwanjani. Ukaguzi utakuwa wa hali ya juu kabla ya kuingia uwanjani.
“Hairuhisiwi mtu yeyote kwenda uwanjani na silaha ya aina yoyote, isipokuwa baadhi ya vyombo vya dola vyenye jukumu la usalama eneo hilo na yeyote atakayekiuka atawajibishwa kisheria” amesema Kamand Muliro
Aisha Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawataka wapenzi na mashabiki wa soka kuwa wastaarabu na kushangilia kwa kiheshima kwa kuzingatia kanuni za uendeshaji wa soka.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawatakia heri ya Pasaka na michezo yote miwili kuwa na mafanikio kwa timu zetu za Simba na Yanga .