Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema Kama ilivyo desturi tunapoelekea kufunga mwaka, kunakuwa na shamrashamra za wananchi kufurahia kumaliza mwaka wakiwa salama na kuingia mwaka mpya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linao wajibu kuhakikisha wananchi wanasherehekea kwa amani na utulivu sikukuu hiyo.
Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP JUSTINE MASEJO amepiga marufu upigaji wa fataki nakuwataka wananchi ambao wanapenda kupiga fataki wafike katika ofisi za Jeshi hilo kupata vibali.