Polisi imethibitisha kuwa baadhi ya walioshikiliwa walihojiwa na kurejeshwa katika mikoa yao walikotoka.

Akizungumza usiku wa kuamkia leo jijini mbeya, Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Polisi, Awadhi Juma alisema baadhi ya viongozi hao ambao walishindwa kukidhi masharti ya dhamana au kuwa na makosa zaidi ya moja au jinai hawajaachiwa.

‘’Jeshi la polisi limewakamata wafuasi wa chama cha Chadema wapatao 145, wakiwemo wakuu wa chama hicho’’.

‘’Takribani watu 520 miongoni mwao viongozi na wafuasi wa chama cha chadema walikamatwa na baadhi kuachiwa huru kwa dhamana,’’ aliongeza.

Mwenyekiti wa taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe, makamu mwenyekiti Tundu Lissu, na Katibu Mkuu John Mnyika ni miongoni mwa waliokamatwa uwanja wa ndege wa Songwe mkoani Mbeya kwa ajili ya kushiriki.