Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Jeshi la Polisi-Kilimanjaro
Jeshi la Polisi nchini limesema limejipanga vyema kuimarisha uzinduzi wa mbio za Mwenge ambazo zinazonduliwa Aprili 2,2024 mkoani Kilimanjaro.
Hayo yamebainishwa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi CP Awadhi Juma Haji akiwa Mkoani Kilimanjaro ambapo amebainisha kuwa Jeshi hilo limejipanga kuimarisha ulinzi wakati wa Uzinduzi wa Mbio hizi.
CP Awadhi amewaomba Wananchi kuhudhuria sherehe hizo ambazo mgeni rasmi atakuwa Mheshimiwa Kassim Majaliwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ameongeza kuwa watu ambao watajaribu kuvuruga amani katika sherehe hizo wasijaribu kufanya hivyo kwani Jeshi hilo watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Kauli mbiu ya Mwenge wa uhuru mwaka 2024 inasema “Tunza mazingira na shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu”
Mwenge wa uhuru uliwashwa kwa mara ya kwanza Mkoani Kilimanjaro na unatimiza miaka 60 tangu kuzinduliwa kwake na muasisi wake Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961 ambaye pia anatimiza miaka 25 tangu kifo chake.