Na Lookman Miraji, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Jeshi la Polisi Wilaya ya Kinondoni limeadhimisha sherehe za miaka 60 ya Kesshi la polisi Tanzania.

Sherehe hizo zimeadhimishwa Septemba 9,2024 katika fukwe maarufu za Coco abeach, Dar es Salaam.

Sherehe hizo zimeadhimishwa na jeshi la polisi wilaya ya Kinondoni ambapo zilienda sambamba na ufanyaji usafi katika fukwe hizo pamoja na utoaji elimu kwa jamii juu mambo mbalimbali ambayo yameonekana kushamiri kwa siku za hivi karibuni.

Akizungumza kwa niaba ya Jeshi la Polisi Wilaya ya Kinondoni, Kamishna msaidizi wa jeshi la polisi ambaye pia ni Afisa mnadhimu wa mkoa wa kipolisi Kinondoni Afande: Pili Misungwi ambaye amesema kuwa kupitia maadhimisho ya miaka 60 ya jeshi la polisi Tanzania , Jeshi la Polisi la limeadhimia kufanya mambo mbalimbali ya kijamii ambayo yangechochea ushirikiano kwa jamii ambapo miongoni mwa mambo hayo ni kufanya usafi katika mazingira yanayoizunguka jamii, utoaji elimu pamoja na kuchangia damu.

“Sisi kama Jeshi la Polisi kupitia maadhimisho haya ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi la Tanzania tumeamua kuungana na jamii kufanya mambo mbalimbali katika jamii ambayo yatachangia kuongeza ushirikiano baina ya jeshi la polisi na jamii.

Leo tumefika hapa fukwe za Coco Beach kwa sababu eneo hili kwetu tunalihesabu kama ni eneo maalumu ambalo pia linasifika kwa mambo mbalimbali ikiwemo ya utalii na lakini linafikiwa pia na wageni wengi kutoka nnje ya nchi na maeneo mengine tofauti. Eneo hili sisi tunalitizama kama eneo ambalo lina uwakilishi wa kiubalozi kwa nchi yetu ya Tanzania.

Tulichagua eneo hili kwaajili ya maadhimisho haya kwani katika maadhimisho haya tuliadhimia kufanya mambo mbalimbali ya kijamii ambayo vingechochea kuleta ushirikiano mzuri na jamii miongoni mwake ikiwa ni pamoja na kufanya usafi wa maeneo mbalimbali katika jamii lakini pia kutoa elimu na kuchangia damu.” amesema Afande Misungwi.

Aidha Afande Misungwi pia amegusia juu ya utoaji wa elimu kwa jamii juu ya mambo ya ukatili wa kijinsia ili kwa pamoja waweze kupingana navyo na hata vinapotokea katika jamii waweze kushirikiana na jeshi la polisi kuwachukulia hatua hatua stahiki wahisika wa matukio kama hayo.

Mbali hayo pia Afande Misungwi ameongeza kwa kueleza kuwa wamekuwa wakiimarisha ulinzi katika eneo hilo kila siku na wataendelea kuongeza nguvu kuhakikisha maeneo yanayozunguka fukwe hizo yanakuwa na usalama wa kutosha kwa nyakati zote.

Naye pia mwakilishi wa wafanyabiashara katika fukwe hizo za Coco akizungumza na Jamhuri digital mara baada ya shughuli hizo kumalizika aliyejitambulisha kwa jina la Razack Kimwaga ameonekana kufurahishwa kwa jitihada hizo zilizofanywa na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanatoa elimu hiyo kwani itasaidia kupunguza vitendo vingi sana ambavyo vimekuwa vikitokea katika fukwe hizo.

Pia ameongeza kuomba wafanyabiashara wa eneo kujitambua kifikra na kutambua nafasi ya jeshi la polisi katika jamii hali ambayo itadumisha ushirikiano na kuongeza amani na usalama kwa watumizi wote wa fukwe za Coco beach.

Katika maadhimisho hayo ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi Tanzania yanaenda sambamba na kauli mbio isemayo “Huduma bora za kipolisi kwa Umma zitapatikana kwa kubadilika kifikra , Usimamizi wa Sheria na matumizi ya Tehama”.

Shughuli za maadhimisho hayo zinatarajiwa kuadhimishwa rasmi kitaifa Septemba 17 mwaka huu 2024.

Please follow and like us:
Pin Share