Kampuni ya PLASCO hivi karibuni itaikabidhi Hospitali ya Taifa Muhimbili msaada wa Tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita laki mbili ambalo thamani yake ni sh. mil.150 ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kampuni hiyo kurejesha kwa jamii.

Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Bw. Ali Gulamhussen amebainisha hayo leo alipofanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi.

“Kampuni yetu huwa ina utaratibu wa kufanya CSR (Kurejesha kwa jamii kila mwaka) mwaka huu tuliwasiliana na Waziri wa Maji Juma Aweso ili atuelekeze mahali pa kupelekea msaada naye alituambia tulete MNH” amesema.

Kwa upande wake Prof. Janabi ameeleza kuwa MNH ina uhitaji mkubwa mkubwa wa maji ambapo kwa siku inatumia lita Milioni moja na laki mbili hadi milioni moja na nusu wakati uwezo wake wa kuhifadhi maji ni lita Milioni moja tu.

“Wakati wa upungufu wa maji huwa tunapata changamoto hasa kwa upande wa kitengo cha kusafisha damu (Dialysisi) kwa kuwa mchakato wa kusafisha damu unahitaji maji safi ambayo siyo ya visima” amesema Prof. Janabi.

Aidha ameahidi kuendelea kushirikiana na kampuni hiyo katika kutekeleza mkakati ya MNH kuanza kuvuna maji ya mvua

Please follow and like us:
Pin Share