Na Mussa Augustine,JamhuriMedia
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda amesema kuwa changamoto zinazokumba Muungano wa Tanzania zinatakiwa kuondolewa ili kulinda Maono ya Waasisi wa Muungano huo ambao hawakutaka kuwepo kwa ubaguzi katika wa Watangangika na Wazanzibar.
Waziri Mkuu Mstaafu Pinda amesema hayo mwishoni mwa wiki kwenye kongamano la Kumbukumbu ya Miaka 23 bila Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambalo limeandaliwa na Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu nyerere Mkoa wa Dar es salaam nakuwakutanisha wadau mbalimbali ili kujadili falsafa za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Amesema kuwa baadhi ya Vikwazo vya Mungano vimeondolewa nakusisitiza kuendelea kuondoa vilivyopo ķwa sasa ili kuhakikisha wanaulinda Muungano wa Tanzania pamoja na watu wake kwani waasisi wa Mungano huo walifanya kazi kubwa kuhakikisha Tanganyika na zanzibar zimeungana kama nchi moja ya Jamhuri.
Amesema kwamba Mwalimu Julias Nyerere Mwaka 1952 alingia kwenye harakati za ukombozi barani afrika nakufanikisha tanganyika kupata uhuru mwaka 1961 ,ndipo alipokutana na Raisi mwenzake wa Zanzibar Hayat Amani Abeid Karume nakukubaliana kuungana ambapo mwaka 1962 waliunganisha Tanganyika na zanzibar nakuwa Jamhuri ya Tanzania hivyo viongozi waliopo madarakani kwa sasa waulinde muungano huo.
“Kama Muungano Mtauvunja Tanzania na Bara mtabaguana kwa kila kitu,hata makabila mtabaguana,mtabaguana kidini,sasa hii hatua ni hatari sana msithubutu kuvuruga muingano” alisisitiza Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda kwenye Kongamano hilo.
Amesema kuwa baba wa Taifa Hayat Mwalimu Nyerere za enzi za uhai wake alihubiri misingi mikuu ya Taifa ambayo ni Amani ,Umoja,na Mshikamano hivyo misingi hii inapaswa kurithishwa kwa vijana ambao bado wana umri mdogo kutunza kumbukumbu ikiwemo vijana wa shule za msingi na sekondali ili kulifanya Taif kuwa na Vijana Wazalendo kwa Taifa leo.
Nimefurahi leo Kwenye kongamano hili mmewashirikisha wanafunzi wenye umri mdogo ,natumaina mada mtakazojadili hapa zitawasaidi vijana wetu kumjua vizuri baba wa Taifa na falsafa zake nakulifanya taifa letu kuwa na vijana wazalendo” alisema.
Kwa Upende wake Mwenyekiti Taifa wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Paul Kimiti alisema kuwa Watanzania waendelee kupigania urithishaji wa misingi iliyoachwa na baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kimiti ambaye amewahi kushika nyazifa mbalimbali kwenye serikali ya Hayati Julius Nyerere ikiwemo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Waziri wa Kilimo, alisema Wadau wajitolee kufanya kazi yakurithisha jamii tunu alizoziacha baba wa Taifa ambazo ni Upendo, Amani, na Mshikamano.
Baadhi ya Wanafunzi wa sekondari Kawe Ukwamani Joha Abdalah na Emmanuel Daffi waliiambia Jamhuri kwa nyakati tofauti kuwa Baba wa Taifa aendelee kuenziwa na kuheshimiwa ,kwani ndiye aliyetupatia uhuru nakulifanya Taifa kuwa na Amani na Utulivu.