Arusha. Madiwani watatu wa chadema katika halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro mkoa Arusha ,wamejiuzuru na kujiunga na chama cha mapinduzi(CCM)
Kujiuzulu kwa Madiwani hao sasa kumeongeza Madiwani wa Chadema waliohamia CCM mkoa wa Arusha ambao wanafikia 15 ndani ya mwaka mmoja.
Madiwani hao, kutoka tarafa ya Ngorongoro mkoani Arusha wamedai kuwa uamuzi wao huo wa kukihama chama cha CHADEMA ni wa kumuunga mkono Rais John Magufuli katika utendaji wake wa kazi.
Madiwani hao ni Daniel Olkery wa kata ya Ngorongoro, Lazaro Saitoti kata ya Ngoile pamoja na Sokoine Moir ambaye ni diwani wa kata ya Alaitole.
Uamuzi wa kujiuzulu Madiwani hao waliotoa katika mkutano wa Mwenyekiti wa CCM mkoa Arusha loota Sanare na Mbunge wa jimbo hilo. William ole Nasha ambaye pia ni Naibu waziri wa Elimu uliofanyika Jana Ngorongoro.
Sanare baada ya kupokea kadi za chadema za Madiwani hao, aliwakabidhi kadi za CCM.
Hata hivyo. Mkurugenzi wa halmashauri ya Ngorongoro, Raphael Siumbu alisema anasubiri barua rasmi za Madiwani hao.
“Hata Mimi nimesoma kwenye vyombo vya habari kujiuzuru Madiwani hao ila tutatambua baada ya kupata barua rasmi” amesema