Na Lookman Miraji

Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) inatarajia kuzindua rasmi ufanyaji wa kazi kwa saa 24 katika tawi lake la Kariakoo, Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi mwendeshaji wa benki hiyo Arafat Haji katika hafla ya ftari ya pamoja iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Dar es Salaam mapema wiki hii.

Aidha mkurugenzi huyo amesema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya kuleta unafuu na urahisi kwa wateja wake kupata huduma za kifedha bila kikwazo kwa wakati wowote watakapohitaji huduma za kifedha.

Hatua hiyo inakuwa muendelezo wa hamasa kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Dar es Salaam kuendesha biashara kwa saa 24.