Papa Francis ameonya dhidi ya kutumia dini kuchochea migogoro katika siku yake ya mwisho ya ziara yake nchini Indonesia, sehemu ya kwanza aliofika katika ziara yake ya kuzunguka eneo la Asia Pacific.

Katika msikiti wa Istiqlal katika mji mkuu wa Jakarta, Papa alitia saini tamko kuhusu maelewano ya kidini na ulinzi wa mazingira na imamu mkuu wa msikiti huo na kukutana na viongozi wa eneo hilo wa dini sita.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 87 mapema Jumanne alianza ziara ya siku 11 katika eneo hilo, safari ndefu zaidi nje ya nchi kama papa.

Baada ya kusherehekea misa mbele ya umati wa watu 80,000 unaotarajiwa katika uwanja mkuu wa kandanda wa Indonesia baadaye siku hiyo, atakwenda Papua New Guinea, Timor Leste na Singapore.

Akizungumza katika msikiti huo – ambao ni mkubwa zaidi Kusini Mashariki mwa Asia – Siku ya Alhamisi, Papa alisema watu kutoka dini tofauti walipaswa kujua “sisi sote ni ndugu, wote ni mahujaji, sote tuko njiani kuelekea kwa Mungu, zaidi ya kile kinachotutofautisha”.

Ubinadamu unakabiliwa na “mgogoro mkubwa” unaoletwa na vita, migogoro na uharibifu wa mazingira, aliongeza.

Indonesia ndiyo nchi yenye Waislamu wengi zaidi duniani na asilimia 3 tu ya milioni 275 ndio Wakatoliki.

Indonesia ina dini sita zinazotambulika rasmi — Uislamu, Uprotestanti, Ukatoliki, Ubudha, Uhindu, na Ukonfusimu.