“Ninyi ni wachungaji, si viongozi wa kijamii wala viongozi wa kisiasa. Hebu tujiepushe na mihemko itakayotufanya kuchanganya huduma ya Mungu na masilahi ya kupita yaliyotiwa chumvi.”
Haya ni maneno ya Baba Mtakatifu Papa John Paul II alipokuwa akiwaasa wachungaji na mapadre kote duniani kutenganisha dini na siasa.
***
Mandela: Viongozi wenye Ukimwi
“Viongozi duniani kote wanaoishi na virusi vya Ukimwi watiwe moyo – si kulazimishwa – kuongoza kwa mifano na kutangaza kuwa wana virusi vya Ukimwi.”
Haya ni maneno ya Rais wa Kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Mandela (95), mwenye mtazamo kuwa viongozi wenye virusi vya Ukimwi wakijitangaza unyanyapaa utapungua katika jamii.
***
Kissinger: Viongozi na umaarufu
“Viongozi wanawajibika si kwa kura za umaarufu pekee, bali pia kwa matokeo ya matendo yao.”
Haya ni maneno ya Mmarekani mwenye asili ya Ujerumani, Henry Kissinger, aliyewahi kushika wadhifa wa uwaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani na kutawala siasa za kimataifa kati ya miaka ya 1969 ya mwishoni hadi mwaka 1977.
***
Olmert: Wanasiasa wanayo nafasi
“Viongozi wa kisiasa wanayo nafasi ya kubadili mitazamo hasi yenye kuasili mahusiano katika jamii.”
Maneno haya aliyasema aliyekuwa Waziri Mkuu wa 12 wa Israel, Ehud Olmert, aliyetawala kati ya 2006 na 2009 aliyekuwa akitafuta uwezekano wa kumaliza mgogoro kati ya Waisraeli na Wapalestina.