Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis amezikwa hii jana mjini Roma, katika mazishi yaliyohudhuriwa na maelfu ya watu wakiwemo viongozi wa dini na marais kutoka kote uliwenguni.
Papa Francis amezikwa kwenye Kanisa alilolichagua la Mtakatifu Maria Maggiore mjini Roma, baada ya misa ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.
Kadinali Giovanni Battista Re aliyeongoza misa hiyo alisisitiza juu ya ujumbe wa Papa Francis wa kuwaunganisha watu badala ya kuwatenganisha na kurejelea ujumbe wa kujenga madaraja, na si kuta.
Viongozi mbalimbali wa dunia walihudhuria, ikiwa ni pamoja na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi, rais wa Kenya William Ruto, rais wa Angola Joao Lourenco na makamu wa rais wa Tanzania Philip Mpango.
