Madaktari wamesema Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis atasalia hospitalini kwa siku nyingine kadhaa.

Taarifa iliyotolewa na Vatican jana Jumatatu ilisema papa Francis anaendelea vizuri na matibabu.

Taarifa hiyo iliongeza Papa Francis licha ya kuonekana kupata nafuu siku chache zilizopita, lakini bado anahitaji uangalizi wa madaktari na kuendelea na tiba.

Kiongozi huyo wa Kanisa mwenye miaka 88 aamelazwa hospitalini kwa zaidi ya wiki tatu sasa kutokana na maambukizi kwenye njia ya hewa.