Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, jana Jumapili ameshindwa kuongoza misa kama ilivyo kawaida yake kutokana na matatizo ya kiafya yanayomsumbua.

Vatican ilithibitisha kupitia taarifa rasmi kwamba Papa Francis hatokuwa na uwezo wa kuongoza misa hiyo kutokana na changamoto ya mfumo wa upumuaji inayomsumbua.

Papa Francis, mwenye umri wa miaka 88, amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa zaidi ya wiki moja sasa na kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Gemelli, Roma, ambapo anaendelea kupatiwa matibabu.

Awali, Vatican ilisema kuwa Papa ataendelea kubaki hospitalini kwa muda utakaothibitishwa na madaktari, huku ikieleza kuwa kwa sasa hali yake inaendelea vizuri.

Taarifa hii ilithibitishwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Vatican, Matteo Bruni.