Kifo cha Papa Francis siku ya Jumatatu akiwa na umri wa miaka 88 kimekuja baada ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki kukumbwa na matatizo kadhaa ya kiafya katika miaka ya hivi karibuni.
Francis alifariki asubuhi Jumatatu katika makazi yake, Vatican ilisema. Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu, Vatican ilisema Francis alifariki kutokana na kiharusi cha ubongo, kukosa fahamu na baadae mshituko wa moyo.
Papa, ambaye sehemu ya pafu moja ilitolewa akiwa kijana, alipambana na matatizo ya kiafya kwa muda mrefu na alikuwa akikabiliwa na magonjwa ya kupumua . Alilazwa hospitalini kwa wiki tano msimu huu wa baridi baada ya kupata nimonia mara mbili.
Mnamo Julai 2021, alikaa hospitalini kwa siku 10 kufuatia upasuaji wa utumbo mwembamba. Machi 2023, alilazwa hospitalini kwa siku tatu. Miezi michache baadaye, Juni 2023, alirudi hospitalini kufanyiwa upasuaji wa wa utumbo.
Tangu 2022, mara nyingi alitumia kiti cha magurudumu, kitembezi au fimbo kutokana na majeraha ya goti, na alikuwa kutokana na kuanguka mara nyingi.
