Latest Posts
Mjasiriamali na nguvu ya fedha
Katika maisha yangu, ninaamini na kusimamia mambo makubwa matatu – ujenzi wa roho, ujenzi wa familia na ustawi wa kiuchumi. Naamini kuwa mafanikio ya kweli katika nyanja zote za maisha lazima yaanzie rohoni mwa mtu.
Ndugu zangu, nchi inateketezwa
Wapendwa, nimeshindwa kujua simanzi hii iliyonipata niielekeze kwa nani. Kilio hiki nakileta kwenu ili kwa pamoja tuweze kupata jibu la hiki kinachojaribu kukieleza hapa.Wiki iliyopita nilisafiri kutoka Dar es Salaam hadi Kyela mkoani Mbeya kwa kutumia gari. Nilirejea Dar es Salaam kwa usafiri huo huo. Njiani nilishuhudia mambo kadhaa ambayo naomba sana ndugu zangu tushirikiane kuyajadili.
Dalili ya kudidimia kwa uongozi bora Afrika
TUZO YA MO IBRAHIM KUKOSA MSHINDI
Nimesikitishwa na habari za Tuzo ya Mo Ibrahim kukosa mshindi mwaka huu, zilizotangazwa hivi karibuni na Kamati ya tuzo hiyo ambayo ni zawadi yenye thamani kubwa dunaini. Tuzo hiyo ilianzishwa mwaka 2006 na bilionea wa nchini Sudan, Mo Ibrahim, kwa ajili ya marais wastaafu wa nchi za barani Afrika.
JKT ni mtima wa Taifa (1)
Nimefurahishwa sana na tamko la Mkuu mpya wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael Muhuga, alilolitoa Ikulu Septemba 26, mwaka huu, mara tu baada ya kuapishwa kwake kushika wadhifa huo.
Ushindi mgogoro Ziwa Nyasa ni wetu – Membe
*Wazee wataka waruhusiwe watumie ‘nguvu za miujiza’
“Inawezekana shetani kaingia. Huku Tanzania tuna uwezo hata wa kutumia ungo…mimi nimekulia hapa, mpaka ni katikati ya ziwa…Kama ninyi (Serikali) hamna bunduki, wananchi wapo tayari kupigana kwa kutumia fito…Hatutakufa mpaka tuone mwisho wa mgogoro huu, tupo tayari hata kwa kutumia miujiuza yetu,” Haya ni maneno ya Mzee Anyosisye Mwakenja (80) wa Kijiji cha Matema Beach.
Hivi haya ya Tanzania ni ‘majiji’ au ni ‘mazizi’?
Wiki iliyopita Tanzania imeongeza jiji jingine kwenye orodha yake. Arusha imeungana na majiji mengine yaliyoitangulia- Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya na Tanga. Mamilioni ya shilingi yametumika kwenye uzinduzi rasmi uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete, wakati wa ziara yake mkoani Arusha. Kitu cha maana zaidi kilichofanywa na Rais Kikwete kwenye ziara hiyo ni uzinduzi wa Chuo cha Nelson Mandela, kitakachosaidia kuibua na kuendeleza vipaji katika fani ya sayansi hapa nchini.