JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Serikali: Vitambulisho vya uraia vinatolewa bure

SERIKALI imewatoa hofu wananchi kwa kuwahakikishia kuwa vitambulisho vya uraia vitatolewa bure kwa Watanzania wote. Msimamo wa Serikali ulitolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa hapo kutoka kwa wabunge.

Rais Kikwete anaihujumu CCM!

Kuna siku nilikuwa eneo moja la katikati ya Victoria na Makumbusho jijini Dar es Salaam, tukijadili mambo mbalimbali likiwamo la matokeo ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki. Hapo kuna mtu aliibua hoja ya hali aliyonayo Rais Jakaya Kikwete kwa sasa.

Bosi TBS hachomoki

*CAG aanika madudu mengine mapya
*Omo, Blueband, mafuta ya ndege hatari
*Pikipiki feki, vinywaji hatari kwa walaji
*Aruhusu Kobil wachakachue mafuta

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ametoa taarifa ya ukaguzi maalumu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), na kuibua mambo ya hatari zikiwamo kampuni za mawaziri zinazoingiza mafuta ya magari yasiyofaa.

Jaji Warioba natarajia urejeshe Tanganyika yetu –2

[caption id="attachment_2" align="alignleft" width="158"]BalileDeodatus Balile[/caption]Wiki iliyopita nilihitimisha makala yangu kwa kukueleza jambo muhimu mpendwa msomaji. Hitimisho langu lililenga katika kukujuza japo kwa ufupi Jaji Warioba ni nani.

Wakubwa wanavyotafuna nchi

[caption id="attachment_27" align="alignleft" width="314"]Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utoah, akiwasilisha ripoti ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha wa 2009/2010 kwa waandishi wa habari bungeni mjini Dodoma, wiki iliyopita[/caption]*Kampuni ya Mohamed Enterprises yauziwa viwanja kinyemela
*Bandari watumbua zaidi ya bilioni 1.5, waendesha miradi hewa
*Mabosi wanachomeka watumishi hewa, wanavuta mishahara

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2011; imeendelea kufichua namna kundi la watumishi wa umma na wafanyabiashara wakubwa wanavyoitafuna Tanzania. Utouh aliwasilisha taarifa hiyo bungeni mwishoni mwa wiki.

Ni vita ya rushwa, haki

Uchaguzi wabunge EALA…

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano leo wanatarajia kuchangua wabunge tisa watakaoiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA).