JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Membe amkamata Kitine pabaya

Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Usalama wa Taifa, Dk. Hassy Kitine, ameshindwa kumtaja waziri anayedai kwamba amechota fedha katika mataifa kadhaa kwa ajili ya kujenga hoteli na kujiandaa kugombea urais mwaka 2015.

Dk. Kitine alipokuwa akihojiwa katika Kituo cha Televisheni cha Channel 10 cha jijini Dar es Salaam hivi karibuni, alidai kwamba waziri huyo ana kiasi kikubwa cha fedha.

‘Nyundo’ ya mafisadi ilipotua Mwibara!

Hii ni hotuba iliyotolewa na Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), kwa wananchi waliompokea Mei 3, 2012 katika eneo la Kibara kwa ajili ya kumpongeza kwa ushujaa wake wa kuwashupalia mafisadi.

Wosia wangu kwa Komredi Kaghasheki

Makomredi Khamis Kagasheki na Lazaro Nyalandu; Salaam. Mlipoteuliwa kuiongoza Wizara ya Maliasili na Utalii wapo waliowapongeza. Mimi nilisita kuwapongeza.

Zitto atoa ya moyoni

[caption id="attachment_62" align="alignleft" width="133"]ZittoMbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe[/caption]Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, mwishoni mwa wiki amefanya mahojiano maalum na Gazeti la JAMHURI kuhusiana na mwenendo wa Bunge na mwelekeo wa taifa hili kwa ujumla. Mwandishi Wetu DEODATUS BALILE anakuletea mahojiano hayo kama ifuatavyo:

Anwani za makazi, vitambulisho vya taifa vina umuhimu wa pekee

Katika toleo la leo tumechapisha habari za mchakato wa kuandaa anwani za makazi (postal code) kukamilika. Mpango huu umeandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na muda si mrefu karibu kila nyumba hapa nchini itakuwa ikitambulika.

Vigogo watafuna nchi

*Wabunge wawili CCM walipwa fidia Sh milioni 964 bado jengo lauzwa
*Zitto asema kalinunua Fida Hussein
*Ataka Katibu Mkuu Fedha ahojiwe

Wakati Rais Jakaya Kikwete amebadili Baraza la Mawaziri kutokana na shinikizo la Bunge, taarifa zimevuja kutoka serikalini kuwa kuna vigogo na watendaji wakuu wanaouza mali za umma kama zao.