JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Pinda akunjua makucha rasmi

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akihutubia Bunge mjini Dodoma hivi karibuniSerikali imesema kuanzia sasa watumishi wabadhirifu wa fedha za umma hawatahamishiwa vituo vingine vya kazi, bali watachunguzwa na ikibainika watafukuzwa kazi mara moja.

Ubingwa wa Euro sasa ni ama Hispania au Ujerumani

* Kompyuta za England kwa Italia ovyo

Kung’olewa kwa England katika robo fainali za michuano ya Kombe la Euro 2012 na kukamilisha idadi ya timu nne ambazo zitacheza nusu fainali, kumeziacha Hispania na Ujerumani zikipewa nafasi kubwa zaidi kwa mojawapo kuwa bingwa.

Katiba Mpya Tanzania Mpya – 10

Mpendwa msomaji wa makala ya Katiba Mpya Tanzania Mpya, nilipoanza kuzungumzia uhuru wa kutoa maoni na suala la Muungano, nilianza kwa kufuatilia historia ya nchi yetu angalau kwa wale wasioijua historia ya Muungano ili wapate kuijua vizuri na kuona ni wapi tulitoka, tulipo na tunakoelekea, lakini pia si tu tunaelekea wapi bali tunaelekea wapi kwa namna gani.

Michezo kikolezo cha ‘jeuri’ ya taifa

Nakumbuka mchakamchaka na mapigo ya bendi ya shule enzi za elimu ya msingi. Mwalimu wa michezo, mwalimu wa zamu na wengine waliokuwa wakipenda ukakamavu walikuwa mstari wa mbele kwenye shughuli hizo kabla ya kuingia darasani.

Mwanasheria Mkuu awamaliza Uamsho

*Asema wanataka kuipeleka Zanzibar vichakani

Mchakato wa kuandika Katiba Mpya umepata hamasa kubwa hasa visiwani Zanzibar. Huko kuna kundi la dini lijulikanalo kama Uamsho. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Othman Masoud Othman, ameamua kuweka mambo sawa kwa kile anachoona jinsi kikundi cha Uamsho kinavyoipotosha jamii. Endelea…

Siku Ngeleja alipowavaa Mbowe, Zitto

Wiki iliyopita, Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (CCM), aliikosoa bajeti ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na kusema kuandaa bajeti ya nchi si sawa na kuandaa bajeti ya harusi.