JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Bilionea akubaliwa kujenga uwanja Serengeti

Mamlaka zote za Serikali zimeridhia ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mugumu, Serengeti mkoani Mara.

Waislamu, Walokole pigeni moyo konde

Kwa karibu miaka miwili sasa nimejiepusha kuandika mada zinazohusiana na masuala ya dini, hasa Uislamu. Niliacha kuandika si kwa sababu nyingine bali kujipa muda niweze kupima upepo, kuangalia mustakabali wa taifa hili na hatimaye kuwa na mawazo muwali yatakayoniwezesha kutoa…

Vigogo wa bilioni 300 wakalia kuti kavu

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema vyombo vya dola vimeanza kuchunguza taarifa za kuwapo kwa zaidi ya Sh bilioni 300 zilizofichwa katika benki nchini Uswisi.

 

Pinda ameliambia Bunge kuwa Serikali imepata taarifa hizo kupitia vyombo vya habari, na kwamba tayari wameanza uchunguzi na baadaye watatangaza matokeo.

 

Twende tuwekeze Sudan Kusini – Jenerali Kisamba

*Saruji, ngano, vifaa vya ujenzi, alizeti vinahitajika

*Asema majirani zetu wameshaanza kunufaika mno

 

Ushauri umetolewa kwa Tanzania na Watanzania kuamka na kuchangamkia fursa za uwekezaji na biashara zilizojitokeza katika taifa jipya la Sudani Kusini.

 

Katiba Mpya, Tanzania Mpya 11

Kama nilivyoahidi wiki iliyopita, kwamba baada ya kuwa tumemaliza kulizungumzia suala la Muungano kwa urefu na upana, ningeanza kuzungumzia suala la ardhi katika Taifa letu na jinsi Katiba ya sasa inavyolieleza suala hilo na umiliki wake kwa Watanzania.

 

Balotelli aichanganya Italia

…Ageuka pia kuwa shujaa barani Afrika

Mapema mwaka huu, Mario Balotelli aliachwa katika timu ya taifa ya Italia (Azzurri) iliyocheza na Marekani Jumamosi, Februari 29, lakini Alhamisi iliyopita ghafla aliichanganya Italia alipoipeleka kucheza mechi ya fainali za Euro 2012 hapo juzi, Jumapili, dhidi ya Hispania mjini hapa.