JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Yah: Nahisi sasa kuwa ni mganga wa kienyeji

Tangu zamani dhana kwamba mtu mzee ndiye mchawi katika jamii, imejengeka sana miongoni mwa walio wengi wenye upeo mdogo wa kufikiri na kuiaminisha jamii yenye maadili mema kuwa na imani potofu kwa sisi wazee.

Vita kubwa TANESCO

*Wabunge wajiandaa kukwamisha tena bajeti ya Wizara ya Nishati, wahoji zabuni ya mafuta BP

 *Wajiandaa kuwang’oa Waziri Profesa Muhongo, Katibu Mkuu Maswi Ijumaa ya wiki hii

 *Katibu Mkuu aanika ukweli, asema Wizara yake haikufanya manunuzi waliohusika ni RITA, Zitto anena

[caption id="attachment_219" align="alignleft" width="243"]Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Peter MuhogoWaziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo[/caption]Kuna kila dalili kuwa imeibuka vita ya wazi kati ya Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), huku Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco aliyesimamishwa kazi, William Mhando, akipigiwa debe la wazi na wabunge.

Taarifa zilizopatikana kwenye ofisi za Bunge zinasema kuwa Kamati ya Nishati na Madini inajipanga kukwamisha bajeti ya wizara hiyo kama Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco aliyesimamishwa kazi, Injinia Mhando, hatarejeshwa kazini huku wizara ikisisitiza kuwa amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wala hajafukuzwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, naye ana msimamo kuwa Mhando ameonewa na wizara inaweza kujiokoa kwa kumrejesha ofisini kisha ufanywe uchunguzi maalumu utakaoendeshwa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).

 

Tuukatae ushoga na ndoa za jinsi moja – 2

Ninachukizwa sana na matamshi ya mara kwa mara kutoka kwa viongozi wakuu wa mataifa ya Magharibi.  Hivi karibuni mkuu wa Marekani ametamka kuwa anaunga mkono ndoa za jinsi moja.

CCM ni kama wameitwa na chunusi

Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde (Chadema) mwanzoni mwa mkutano wa Bunge unaoendelea sasa, alizungumza maneno ya hekima.

 

Akieleza safari ya kifo cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) alifananisha hali hiyo na tajiri anayefilisika. Akasema tajiri anayefilisika huwa hajitambui, na kwamba akijitambua kuwa anafilisika, kamwe hatafilisika. Hatafilisika kwa sababu atajitahidi kutafuta mbinu za kujikwamua. Akasema kwa hali ya mambo ilivyo, CCM haijitambui kama inakufa, na kwa sababu hiyo, inakufa!

Yah: Haiwezekani Mtanzania abaguliwe ndani ya Tanzania

Wanangu, naamini mu bukheri wa afya na mnaendelea kufanya kazi kwa bidii kama tulivyokuwa tukifaya sisi wakati wa ujana na afya zetu.

Yah: Tulianza kusimama dede sasa tunabebwa.

Wanangu nianze kwa kuwapa kongole kwa kazi za kuliendeleza taifa ambalo linamkosi mkubwa na jambo linaloitwa maendeleo, linamkosi kwa sababu kwa kipindi cha miaka hamsini ya tangu kuzaliwa kwake bado linachechemea, kwa ufupi ndio kwanza linaanza kusimama dede ili lipige hatua ya kwanza lakini dalili zote za kushindwa zinajidhihirisha.