Latest Posts
Kennedy: Tusiichekee vita
“Mwanadamu anapaswa kumaliza vita, vinginevyo vita itammaliza mwanadamu.”
Haya ni maneno ya Rais wa 35 wa Marekani aliyeuawa mwaka 1963. John F. Kenney alikuwa akiamini kuwa dunia inaweza kuwa salama zaidi kwa kutoendekeza vita.
Hongera Mkapa, Kikwete alijiandalia aibu ya Mahalu
Napata wakati mgumu. Napata shida jinsi ya kuanza makaha haya. Napata shida si kwa sababu nina maslahi binafsi, bali kwa sababu nakumbuka hadithi ya mwanafunzi aliyebeba upodo huku akijifunza kurusha mishale ya sumu. Hakuwa mahiri na hakujua jinsi ya kuvuta upinde. Kwa kicheko kikubwa, aliipaka sumu ncha ya mshale, upinde akauelekeza karibu na tumbo lake, kamba ya kurushia mshale ikatokea mbele yake.
Barua ya kibiashara kwa BRELA
Baada ya kuandika makala ya “Biashara za sasa zinahitaji u-sasa”, kuna jambo nililitazamia ambalo limetokea kama yalivyokuwa matarajio yangu. Kumekuwa na wasomaji wengi nchi nzima ambao wameleta maombi na ushauri wakitaka niwasaidie kusajili biashara zao katika mfumo wa kampuni.
Ni aibu TFF, ZFA kugombea Sh milioni 12 za mgawo wa BancABC
Wiki iliyopita, Shirikisho la Kandanda Tanzania (TFF) lililazimika kuutolea ufafanuzi mvutano wa mgawo wa fedha za michuano ya BancABC Super 8 kati yake na Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA), kilipotishia kuziondoa timu zake. Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa fedha zote zilizotolewa na wadhamini wa michuano hiyo – BancABC – zimelipwa kila sehemu kunakohusika zikiwamo timu zote zinazoshiriki, viwanja vinavyotumika, miji inakochezwa na promosheni ya masoko iliyogharimu shilingi milioni nane.
Olimpiki: Kweli kupanga ni kuchagua
Leo nimeazima busara ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliyesema kwamba kupanga ni kuchagua.
Uongozi wa Mwalimu Nyerere haujapata kutokea, si Tanzania tu bali katika nchi nyingi za dunia, hata kama katika hili kuna wale wasioambilika. Kama mipango yote aliyokuwa ameisuka na kuanza kutekeleza Mwalimu ingepata wasimamiaji wazuri, nakuapia leo tungeweza hata kuandaa michezo ya Olimpiki.
Denis Vedasto: Mjasiriamali aliyekuta na JK
“Niliona ni vyema nikuze kipaji changu kuliko kitumike na watu wengine kwa kuajiriwa, kwani nina ubunifu mkubwa kuliko ndiyo maana niliona ni bora nianzishe kampuni yangu.” Hayo ni maneno ya Denis Vedasto, mkazi wa Kitunda, Dar es Salaam ambaye ni mjasiriamali anayejishughulisha na utengenezaji wa vitanda vya hospitali, ambavyo vingine hutumiwa wakati wa kinamama kujifungua.