Latest Posts
Kufuru Katiba Mpya
*Kila mjumbe wa Tume analipwa Sh milioni 294
*Waziri Chikawe asema hizo wanalipwa ‘vijisenti’
*Hofu yatawala kama posho nono hazitawapofusha
*Jaji Warioba, Profesa Baregu wapata kigugumizi
Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Waziri Mkuu (mstaafu) Jaji Joseph Warioba imetengewa mabilioni ya fedha kwa kiwango cha kutajirisha wajumbe wa Tume hiyo ambapo kila mjumbe anapata Sh milioni 294 ndani ya mwaka mmoja.
Ronaldo atamng’oa Messi, kuwa bora duniani?
Zikiwa zimebakia wiki tatu kabla ya Shirikisho la Kandanda Duniani (FIFA) kutoa tuzo ya Mwanasoka Bora kwa mwaka 2012/2013, mashabiki na wadau mbalimbali wa mchezo huo wanaendelea kubishana kuhusu nani anastahili kutwaa tuzo hiyo kati ya wachezaji mahiri watatu waliofika fainali.
Nyerere: Tuoneshe demokrasia kivitendo
“… ingawa kwa nadharia muundo wa Chama chetu (akimaanisha CCM) ni wa kidemokrasia, lakini katika vitendo hatuonyeshi demokrasia wakati wote na kwa shughuli zetu zote.”
Maneno haya ni ya Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambayo ni sehemu ya wosia wake wa kuitaka CCM ijenge dhana ya kuonesha demokrasia ya kweli kwa vitendo.
UN na jitihada za kuisaidia Tanzania
Tanzania ni nchi tajiri kwa rasilimali, na licha ya pato lake kukua mwaka hadi mwaka, wananchi wake ni maskini.
Nguvu ya rangi katika biashara zetu
Leo nitawapitisha wajasiriamali katika somo muhimu kuhusu rangi. Je, unafahamu chimbuko la neno yeboyebo hapa nchini? Twende pamoja. Miaka michache iliyopita, kampuni moja ya hapa Tanzania ilitambulisha bidhaa zake za juisi zilizokuwa zikifahamika kama “Yebo”. Juhudi kubwa ilielekezwa katika kuitangaza…
Nashukuru, utabiri kwa Nyalandu unatimia
Tangu mapema kabisa nilishasema kwamba Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ni tatizo. Niliyasema haya wiki kadhaa baada ya kuteuliwa kwake kushika wadhifa huo.Nyalandu alianza matatizo tangu akiwa Wizara ya Viwanda na Biashara. Nadhani Dk. Cyril Chami, anaweza kuwa msaada mzuri katika hili ninalolisema.