JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Bila kudhibiti NGOs Loliondo haitatulia

Kwa mara nyingine, Loliondo imetawala kwenye vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi. Sina desturi ya kuitetea Serikali, lakini hiyo haina maana kwamba inapoamua kufanya jambo la manufaa kwa vizazi vya sasa na vijavyo, nishindwe kuitetea.

BAADA YA KUANIKA MADUDU…

Ofisi ya CAG sasa yasambaratishwa

 

*Naibu CAG aondolewa, Utouh atakiwa ajiandae kung’atuka

 

Hasira za watendaji kadhaa wa Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Mashirika ya Umma na taasisi mbalimbali dhidi ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, zimeanza kuzaa matunda baada ya kuwapo mpango wa kuwang’oa viongozi wake wakuu.

NuKUU ZA WIKI

Nyerere: Miiko ya uongozi

“Siku hizi fedha ndio sifa kubwa ya mtu kuchaguliwa kuwa kiongozi. Miiko ya uongozi ambayo ni jambo la lazima katika kila nchi duniani, haipo tena hapa nchini.”

Maneno haya ni ya Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Dk. Wande alilia mshikamano Simba

*Ahofu mgogoro wa Simba utaathiri soka nchini

Mwanachama wa siku nyingi wa Wekundu wa Msimbazi, Simba Sports Club ya Dar es Salaam, Dk. Mohamed Wande, ametaja mbinu pekee ya kuinusuru klabu hiyo isididimie kisoka kuwa ni mshikamano wa wanachama na wachezaji.

Udini sasa nongwa (5)

Katika makala iliyopita kwenye safu hii, tuliandika kwa makosa kuwa makala ile ingekuwa hitimisho. Tena kukawa na kosa lililoonyesha kuwa ilikuwa sehemu ya tano. Usahihi ni kwamba hii ndiyo sehemu ya tano na ya mwisho katika mfululilo wa makala hii…

Serikali nayo inapokuwa mlalamishi…

Serikali imesema kasi ya ongezeko la idadi ya watu jijini Dar es Salaam, inatisha. Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Dar es Salaam inakadiriwa kuwa na watu milioni 4.3.