JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Napata wasiwasi kuhusu upotoshaji huu

Nimesoma makala katika gazeti moja litolewalo kila siku, yenye kichwa cha habari, “NIDA imemdhalilisha Rais, majeshi iombe radhi”. Katika makala hayo, mwandishi amejitahidi kuueleza umma kile anachoamini ni ukweli, wa taarifa zilizotolewa katika vyombo vya habari nchini na baadaye kuja kufafanuliwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), kuhusu sakata la vyeti 948 vya majeshi yetu kuwa feki (kughushi).

NIDA waungwe mkono wanafanya kazi muhimu

[caption id="attachment_80" align="alignleft" width="160"]MaimuMkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu[/caption]Vitambulisho vya taifa ni kitu muhimu sana katika ustawi na maendeleo ya taifa letu. Kukamilishwa kwa mchakato wa vitambulisho vya taifa kwa Watanzania na wageni mbalimbali hapa nchini, ni juhudi na mafanikio makubwa ya Serikali na watumishi waliojitoa kwa nguvu na maarifa yao yote kufanikisha azma hii.

Hujatokwa machozi? Zuru wodi 22

Mapema mwezi huu nimejikuta nikiingia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Hii si mara yangu ya kwanza kufika katika hospitali hii kubwa kuliko zote nchini mwetu.

INAKUWAJE MNAMPA “SHETANI” UMAARUFU? (2)

Wiki iliyopita nilieza kwa sehemu namna wachambuzi na wahubiri wengi wanavyoeleza habari za shetani (Freemason, Illuminat, n.k) katika mitazamo hasi kiasi ambacho hofu imetanda miongoni mwa jamii. Ilivyo sasa ni kuwa watu wengi wamebaki njia panda, hawajui cha kufanya baada ya kugundua kuwa kila wanachokigusa ama kinachowazunguka kimebandikwa hatimiliki ya Freemason ama jumuiya nyingine za waabudu shetani.

Kwa nini watu wanashitakiwa kabla upelelezi haujakamilika?

Moja ya mambo yanayosababisha mrundikano mkubwa wa mahabusu magerezani, ni tatizo la watu kushitakiwa mahakamani halafu wanakosa dhamana au kushindwa kutimiza masharti magumu.

NMB wafundisha uelewa masuala ya kifedha kwa wanafunzi

*Moto waanzia Pugu, Mlimani, sasa kuenea nchi nzima
*Unalenga kuwafunza watoto faida za kutumia benki

Benki ya NMB mara zote imekuwa mbele katika kubuni na kutekeleza miradi mbalimbali, yenye lengo la kuwainua Watanzania kimaisha.