JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Siri kifo cha Nyerere

Juhudi za chini chini zimeanza kufanywa na baadhi ya Watanzania ambao hawajaridhika kuwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alifariki kifo cha kawaida.

Nyerere: Vipimo vya utajiri

“Kupima utajiri wa taifa kwa kutumia vigezo vya pato la taifa ni kupima vitu, si ufanisi.”

Haya ni maneno ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyoyatoa Januari 2, 1973 jijini Khartoum, Sudan katika mkutano wa kuimarisha pato la taifa kwa nchi za ukanda wa kusini mwa Jangwa la Sahara.

Wasindikizaji Ligi Kuu Bara wajulikana

 

Wakati Simba Sports Club ikiendelea kuongoza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara hadi mwishoni mwa wiki, timu za Toto African, Ruvu Shooting, Polisi Morogoro na Mgambo Shooting bado zinashindana mkiani zikionesha dalili za kuwa wasindikizaji msimu huu.

Akrama anavyoshutumiwa mechi ya Simba, Yanga

Jumatano iliyopita timu za Simba na Yanga zilishindwa kuoneshana ubabe, baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kabla ya mchuano huo, Simba ilikuwa ikipewa nafasi kubwa ya kushinda hasa kwa vile iliingia uwanjani ikiwa imeshinda michezo yote minne ya awali, huku Yanga ikiwa imeshinda miwili na kufungwa mbili pia.

Afadahi ya ‘ngangai’ kuliko ‘magwanda’ haya (2)

Lema akashinda. Lakini kutokana mwenendo wa kampeni ulivyokuwa, makada wa CCM ambao hawakuridhika, wakafungua kesi Mahakama Kuu na Lema akapigwa chini. Kama kawaida, wafuasi wa Chadema wakiwamo wana harakati na baadhi ya wasomi, wakamsuta Jaji aliyetoa hukumu hiyo kwa madai kuwa ilifanyika kisiasa.

Tunacheza Ziwa Nyasa linaondoka!

Rais Jakaya Kikwete akiwa katika mkutano wa SADC nchini Msumbiji, alimhakikishia Rais Joyce Banda wa Malawi kuwa kamwe Tanzania haitaingia vitani dhidi ya ndugu zao, Malawi.