Latest Posts
Wanawake ni injini ya ujasiriamali
Wakati fulani nilikuwa nikisikiliza wimbo ulioimbwa na mwanamuziki nguli, Luck Dube, na ukatokea kunivutia sana kutokana na maudhui yake. Ndani ya kibao hicho, Dube anaeleza namna wanawake wanavyopambana na maisha kupitia kujituma kuhakikisha familia zao zinastawi vizuri. Hata…
Mwalimu Nyerere na usawa katika jamii
Taifa letu kwa sasa linapita kwenye misukosuko ya udini, ukabila, ukanda na utegemezi. Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, hakusita kamwe kukemea kwa nguvu zote utengano huo, na kusisitiza nchi kujitegemea.
NUKUU ZA WIKI
Nyerere: Jeshi letu ni la Kizalendo
“Jeshi letu haliwezi kuwa Jeshi la mamluki, ni Jeshi la Kizalendo. Matumaini yangu ni kwamba Jeshi letu litaendelea kulinda na kutetea misingi mikuu ya Azimio la Arusha.”
Maneno haya ni ya Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambaye pia ni mwasisi wa Azimio la Arusha.
Polisi wachunguze tuhuma hizi
Habari kubwa katika toleo la leo inahusu mtandao wa mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Liberatus Barlow. Ndani ya habari hiyo, gazeti hili la JAMHURI linamtaja mtuhumiwa Mohamed Edward Malele, Mkazi wa Kijiji cha Igoma, Wilaya ya Kwimba, mkoani Mwanza anayekisiwa kuwa na umri wa kati ya miaka 30 hadi 40 kuwa anashikiliwa na dola.
Lipumba, Limbu wamponda Spika
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema staha ya Bunge itazidi kuporomoka ikiwa utaratibu wa kumtumia Spika anayetokana na chama cha siasa hautabadilishwa.
Tumeirejesha JKT, sasa tuifufue Chipukizi
Wiki iliyopita nilizungumza na wabunge wawili-Martha Mlata na Wiliam Ngeleja, kwa nyakati tofauti. Hawa ni miongoni mwa wabunge waliokuwa ziarani China.
Nilimwuliza, Mlata ni mambo gani yamemvutia baada ya kuiona China . Kabla ya kujibu, uso wake ulionesha namna alivyopata shida ya “aanze kuzungumza lipi”. Aanze kuzungumzia flyovers alizoona, azungumzie kilimo au anieleze kuhusu uzalendo wa Wachina kwa Taifa lao.