Latest Posts
FASIHI FASAHA
Watanzania tunakinyanyasa,
tunakibeua Kiswahili – 7
Sina budi kutoa shukrani kwa wale wote walioniunga mkono katika mada hii ya Watanzania tunakinyanyasa na kukibeua Kiswahili. Ni dhahiri Watanzania wanatambua na wanajali lugha yao ya Kiswahili. Asante. Baadhi ya Waswahili wanasema kuwa lugha ya kaya, kabila, rika, masikani na vijiweni, na hata sehemu zetu za kazi, au michezo zisiwe ni vigezo kuwa Watanzania hawakithamini Kiswahili. Hizo ni lugha za msimu tu.
FIKRA YA HEKIMA
Wawekezaji wazawa waungwe mkono
Watanzania tumejenga kasumba mbaya ya kuwathamini wawekezaji wa kigeni. Wakati huo huo tumekuwa kikwazo kwa wawekezaji wazawa!
Wabunge wa CCM wameshindwa kazi?
Sina sababu yoyote ya kuwavunjia heshima wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Lakini katika enzi hizi za ukweli na uwazi sioni, sababu ya kusita kuzungumzia masuala nyeti kwa ukweli na uwazi. Lengo langu ni kuwaomba waone ugumu wa uchaguzi wa mwaka 2015.
Kashfa zimelilemea Jeshi la Polisi
Wakati fulani wabunge waligombana na aliyekuwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Omar Mahita. Hoja ilikuwa kwamba Jeshi la Polisi lilistahili kuvunjwa ili liundwe upya. Wakatoa mfano wa Jeshi la kikoloni la King African Rifles (KAR), lilivyovunjwa baada ya maasi ya mwaka 1964 na kuundwa kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Wachochezi wa vurugu waadabishwe ipasavyo
Wiki iliyopita, Jeshi la Polisi lilitangaza kumtia mbaroni mtu anayedaiwa kuwa kinara wa kusambaza ujumbe wa kuchochea chuki na uhasama hapa nchini, kupitia simu za kiganjani.
Stars tupeni raha Watanzania
Timu ya Soka ya Taifa (Taifa Stars) inatarajiwa kushuka dimbani Juni 8 mwaka huu, kucheza na Morocco katika mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki Mashindano ya Kombe la Dunia 2014 yatakayopigwa nchini Brazil.