Latest Posts
Vidonda vya tumbo na hatari zake (1)
ijmc
Miili yetu hutegemea vyanzo viwili vya nguvu ambavyo ni oksijeni na vyakula. Oksijeni huingizwa ndani ya miili yetu kupitia pumzi na kuingia moja kwa moja katika utendaji, wakati chakula hutakiwa kupitia mchakato mrefu kuweza kutumiwa na mwili.
Kijana Malele adhalilishwa kutangazwa kichaa
Kijana aliyejitangaza kung’atuka ushirika wa mtandao unaodaiwa kuhusika kumuua Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, anaweza kulalamikia kitendo cha kudhalilishwa kwa kumtangaza kuwa ni mgonjwa wa akili.
Mil 200/- zatafunwa ‘mradi hewa’ Geita
Shilingi milioni 200 zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa skimu ya umwagiliaji katika vijiji vya Nyamboge kilichopo Kata ya Katoma; na Nzera katika Kata ya Nzera, Wilaya ya Geita mkoani, ‘zimeyeyuka’.
Mengi aanzisha shindano kukabili umaskini Tanzania
. Watu wanatuma mawazo bunifu kupitia Tweeter
. Washindi wazawadiwa Sh mil 1.8 kila mwezi
Katika juhudi za kutafuta ufumbuzi wa umaskini Tanzania, Mwenyekiti wa kampuni za IPP, Dk. Reginald Mengi, ameanzisha shindano la mawazo mapya yanayotaja mbinu bora za kutokomeza tatizo hilo.
Tanganyika inarejea, TAKUKURU iko wapi?
Wiki iliyopita Tume ya Marekebisho ya Katiba ilitangaza rasimu ya kwanza. Rasimu hii ina kila sababu ya kusifiwa. Nilipata fursa ya kuwakilisha Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kwa kuchambua na kuwasilisha mapendekezo ya tasnia ya habari nchini. Kwa ufupi nasema, asanteni wajumbe wa Tume kwa kusikiliza kilio cha Wanahabari.
Maisha ya mjasiriamali baada ya kustaafu
Wiki iliyopita nilifika katika mmoja ya mifuko ya pesheni kujiandikisha kwa ajili ya utaratibu wa kujiwekea akiba kwa mpango wa kuchangia kwa hiari. Baada ya kutoka katika ofisi za mfuko huo wa pesheni nikiwa na fomu na makabrasha mengi, nikakutana na mtu mmoja ambaye maongezi kati yangu na yeye ndiyo yaliyonisukuma kuandika makala haya.