JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Sisi bodaboda wao wachukue madini

Wiki iliyopita niliandika maono yangu juu ya kifo cha Tanzania. Nimepata ujumbe wa maandishi na simu nyingi. Wapo walioniunga mkono, wengine wamenishambulia. Kwangu, yote ni heri, kwani hiyo ndiyo faida ya demokrasia na uhuru wa kutoa mawazo.

Kenya, Malawi zilivyolingana nguvu

Timu za soka za Malawi na Kenya, wiki iliyopita zilidhihirisha kulingana nguvu kwa kufungana mabao 2-2 mjini Blantyre, katika mechi ya kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia.

Serikali tatu ni utashi wa kisiasa

Gumzo la kudai kuwa na muundo wa Serikali tatu haukuanza leo. Kwa wafuatiliaji wa mambo ya historia watakumbuka sakata la madai ya kuwa na serikali tatu yaliyoongozwa na Mbunge machachari wa Lupa enzi hizo, Njelu Kasaka, kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam chini ya kivuli cha kundi lililojiita G 55. Waziri Mkuu mstaafu John Malecela anakumbuka kilichomsibu.

Tuwe makini ugawaji mikoa, wilaya

Rais Jakaya Kikwete ametoa baraka za ugawaji Mkoa wa Mbeya ili ipatikane mikoa miwili.

Tayari ameshafanikisha uanzishaji mikoa minne ya Simiyu, Njombe, Katavi na Geita. Pamoja na mikoa hiyo, ameanzisha wilaya nyingi mpya.

Soka la Tanzania bado – Mwaisabula

Kocha mahiri wa soka nchini, Kenedy Mwaisabula ‘Mzazi’, amesema Tanzania bado ina safari ndefu ya kufikia mafaniko katika soka  kwa kulinganisha  na za Ulaya.

NYUFA KATIKA KUTA ZA POLISI

Baba wa Taifa, Mwalimu Juliua Kambarage Nyerere, aliliasa Taifa kuendelea kuchunguza kuwapo kwa nyufa na kuziziba zitokeapo katika kuta za ‘Nyumba’ ya Taifa.