JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Halmashauri ya Geita yatafunwa

* Sh mil 763.8 zakwapuliwa kifisadi

* Mwenyekiti CCM Mkoa ahusishwa

* Waandishi wa habari wapata mgawo

Siku chache baada ya gazeti hili kuchapisha taarifa za nyaraka zinazoonesha Halmashauri ya Wilaya ya Geita ilipokea Sh bilioni 11.1 za kununua madawati lakini fedha hizo hazijulikani zilivyotumika, taarifa nyingine zimepatikana zikionesha ubadhirifu wa Sh zaidi ya milioni 763 katika halmashauri.

Tume ya Katiba inataka kutudhulumu?

Mhariri,

Mimi ninaitwa Issa Juma Dang’ada, ninaishi mjini Nzega, mkoani Tabora. Ni Mjumbe wa Baraza la Katiba Wilaya ya Nzega.

Mwandishi wa barua ile si Mwislamu

 

Mhariri,

Kero yangu ni kwamba ninapinga Barua ya Wasomaji iliyochapishwa kwenye gazeti hili wiki iliyopita. Barua ile imejaa uongo, unafiki na uzandiki. Waislamu wa leo si wa kupelekeshwa na media propaganda.

FRANCIS MBENNA:

Brigedia Jenerali (mstaafu) wa JWTZ anayetimiza umri wa miaka 83

* Atoboa siri ya mafanikio yake

Kesho ni siku muhimu kwa Brigedia Jenerali (mstaafu) Francis Xavier Mbenna, anayetimiza umri wa miaka 83 ya kuzaliwa. Mwanajeshi mstaafu huyu, mkazi wa jijini Dar es Salaam, alizaliwa Julai 31, 1930 huko Likese Masasi, mkoani Mtwara.

Tumepoteza lengo la Siku ya Mashujaa

 

Katika kuwajali mashujaa waliopigania Uhuru na heshima ya Tanzania mwaka 1968, Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha TANU chini ya uongozi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, iliamua kuweka siku maalum ya kuwaenzi mashujaa hao. Ikachaguliwa Septemba Mosi kila mwaka iwe Siku ya Mashujaa Tanzania.

 

KONA YA AFYA

Vidonda vya tumbo na hatari zake (7)

Wiki iliyopita, Dk. Ibrahim Zephania alizungumzia bakteria aina ya H. Pylori na madhara yake ndani ya tumbo la binadamu, na dawa ya vidonda vya tumbo. Sasa endelea kumfuatilia zaidi katika sehemu hii ya saba…

Sigara: Watu wanaovuta sigara/tumbaku ni rahisi kupata vidonda vya tumbo kuliko wasiovua, na vidonda vyao hupona polepole zaidi. Sigara huchoma kunyanzi za tumbo na kuzifanya ziwe rahisi kushambuliwa na asidi.